Tuesday, September 13, 2011

TFF YAWEKA BAYANA JUU UUZWAJI WA TIKETI


                                            
Shirikisho la soka nchni TFF Limesema kuwa limeaandaa utaratibu maalumu wa kuuza tikezi katika uwanja wa Azam ulioko chamazi jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwaondolea usumbufu mashabiki ambao wanakwenda kwenye mechi hizo sambamba na kupunguza vurugu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilifanya uhakiki na kubaini Uwanja wa Azam wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 5,000 tu na si 7,000 kama ilivyoelezwa awali.
Hata hivyo lengo la mmiliki wa uwanja huo ni kuongeza viti hadi kufikia 7,500.

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema tiketi zitakazouzwa kwa mechi za Yanga na Simba kwenye uwanja huo ni 5,000 tu na tiketi zitauzwa siku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mchezo na sehemu zitakuwa ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha Mafuta cha OilCom kilichoko Ubungo na Mbagala Rangitatu. 

Amevitaja viingilio kwa mechi za timu hizo zitakazochezwa Uwanja wa Azam ni sh. 20,000 kwa jukwaa kuu lenye uwezo wa kuchukua watazamaji 400 wakati majukwaa ya kawaida itakuwa sh. 7,000. Ili kuhakikisha idadi ya mashabiki haizidi uwezo wa uwanja hakutakuwa na tiketi za bure (complimentary).

 Ameongeza kuwa kutokana na kuwepo vituo vya kuuzia tiketi katika maeneo yaliyotajwa, mashabiki ambao watakosa tiketi hawana sababu ya kwenda uwanjani. 

Simba na Yanga zitaanza kuutumia uwanja huo kesho (Septemba 14 mwaka huu) kwa Simba kuwa mwenyeji wa Polisi Dodoma wakati siku inayofuata Yanga itakuwa mgeni wa African Lyon.

No comments:

Post a Comment