Tuesday, September 13, 2011

AC MILAN KUMKOSA IBRAHOMOVIC LEO


                                 
Mshambuliaji wa AC Milan Zlatan Ibrahomovic atakosa mchezo wa leo dhidi ya FC Barcelona baada ya kupata jeraha katika mazoezi  na timu yake siku ya jumatatu.

Lakini pia jana tulizungumza kuhusu Arony Ramsey ambaye pia atakosa mchezo wa leo dhidi ya Dotmund baada ya kupata majeraha katika mazoezi na timu yake.

Mshambuliaji huyo raia wa weden mwenye umri wa miaka 29 alieitumikia klabu ya FC Barcelona mwaka 2009-2010 anasumbuliwa na tatizo la misuli lililompata katika maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo wa leo.

Baada ya kuumia kwa mchezaji huyo mkurugenzi wa AC Milan Adriano Galliani amesema hali hiyo haiwapi mawazo makubwa  na hawawezi kulia kutokana na hilo kwa kuwa kunawachezaji wengine watakao ziba pengo la nyota huyo kama Alexander Pato, Antonio Cassano wote wanaweza kucheza.

Aidha taarifa toka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa tatizo la Ibrahomovic litagharim siku chache kupona na baadae kuendelea na kazi kama kawaida.

Mbali na hiyo nyota mwingene wa kibrazil Robinho atakosa mchezo huo kutokana na tatizo la misuli
Kwa maana hiyo kocha wa AC Milan Massimo Allegri atalazimika kuwatumi Cassano na Pato ili kusafisha safu ya ushambuliaji.

Taarifa njema katika klabu hiyo ni kurudi kwa Gianluca Zambrota Clarence Seedorf na Taye Taiwo ambao wote watakuwemo katika mchezo wa leo.
                                     

Wakati AC Milan ikihaha kwa kuuguza majeruhi jana bosi wa mabingwa wa klabu bingwa ya ulaya ambayo ni Barcelona na kocha wake, Pep Guadiola aliwachukuwa nyota 19 wa klabu yake na kwenda kwenye hoteli yenye hadhi ya chini ya La Frolida, baada ya kumaliza mazoezi ya jioni tayari kabisa kuanza ligi ya mabingwa barani ulaya katika uwanja wao wa nyumbani.

Guadiola alikuwa na lengo la kuwajenga nyota hao kisaikolijia mara baada ya miezi minne tangu waibomoe Real Madrid katika uwanja huo kwa mchezo wa nusu fainali ya klabu bingwa barani ulaya.

Lakini pia Barcelona itaingia uwanjani ikiwakosa nyota wake Alex Sanchez na Gerrad Pique kutokana na kukabiliwa na majeraha 

Lakini inasadikiwa  kuwa huenda Guadiola akamtumia Marc Munesa ambaye ni mlinzi wa timu B, alieonekana akiwa katika mazoezi ya pamoja na kikosi cha kwanza na cha Barcelona.

Guadiola amemuongeza Jose Manuel Pinto kipa namba mbili wa timu hiyo alimaliza adhabu yake aliyoipata katika mchezo wa pili wa nusu fainali dhidi ya Madrid baada ya kukwaruzana na benchi la ufundi la madrid. Na adhabu yake ilimalizika katika mchezo dhidi ya FC Porto katika fainali ya uefa super cup.

No comments:

Post a Comment