Lakini pia kule Arsenal Arsene Venga anaamini kuwa mlinzi mpya wa klabu hiyo Per Martsacker ataisadia Arsenal katika mchezo waleo kutokana kucheza ligi ya ujerumani kwa muda mrefu.
Arsena usiku huu inaanza kucheza na Dotmund katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa ikiwa ugenini huku ikiwa na hamasa ya kushinda mchezo mmoja wa ligi dhidi ya Swansea siku ya jumamosi.
Wenga anaamini kuwa mchezo wa kufuzukuingia hatua ya makundi ligi ya mabingwa uliichanganya timu yake hadi kufikia kuharibu michezo ya kwanza ya ligi lakini anaamini maajabu yaleo dhidi ya Dotmund yatarejesha hali ya kujiamini katika kikosi chake.
Amesema ligi ya mabingwa ina atharai kubwa katika kufanya vizuri katika ligi na anafikiri walichanganyikiwa kwa kuondoka nyota wawili kwa mpigo ambao ni samir nasri na Cesc Farbegas.
Ilipelekea timu hiyo kupoteza michezo miwili muhimu dhidi ya United na Liverpool na sasa anaimani ya kuwa wako vizuri na ni wakati wakuonyesha kama wanaweza kufanya vizuri katika ramani ya soka.
No comments:
Post a Comment