Tuesday, September 13, 2011

NITABADILISHA KIKOSI KIDOGO


                                
Kocha wa Chelsea Andre Vila Boas amesema atafanya mabadiliko katika kikosi kitaachoanza leo na Bayern Leverkusen katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani ulaya.

Amesema ni vizuri kushinda michezo yote lakini mabadili hayo yanazingatia umuhimu wa mchezo wa jumapili dhidi ya Manchester united katika mbio za ligi kuu ya England.

Boas amesema mwishoni mwa wiki hii aliwatumia wachezaji wengi aliyakuwa wanauchovu wa michezo ya timu zao za taifa japokuwa waliifunga Sunderland magoli mawili kwa moja.

Aliongeza kuwa mchezo wa leo ni muhimu lakini united ni muhumu zaidi na sivizuri kupoteza kwa hiyo atafanya mabadiliko ili kuondoa uchovu kwa wachezaji wake.
                              
Mlinzi wa Manchester united, Rio Ferdinand hakusafiri na kikosi kilichoelekea Ureno kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa  barani Ulaya dhidi ya Benfica siku ya Jumatano.

Kuachwa kwa nyota huyo si kama ameumia ila Ferdinand amepumzishwa  yeye na Nemanja Vidic kwaajili ya mchezo wa jumapili dhidi ya Chelsea

Kwa maana hiyo Jonny Evans itambidi kwa mara nyingine ashirikiane na Phil Jones kuimarisha safu ya ulinzi katika mchezo huo wa kesho dhidi ya Benfica kule mjini Lisbon.

Ingawa Ferdinand na Vidic bado wataendelea kuwa chaguo la kwanza katika safu ya ulinzi wa kati kwa Manchester United, timu hiyo haijakumbwa na matatizo ilipowakosa wachezaji hao, wakati Ferdinand alipokuwa na matatizo ya mgongo huku Vidic akiwa ameumia misuli gotini.

Wakati walipokuwa wakijiuguza, Evans na Jones wamekuwa moyo wa ulinzi ambapo Man United walifungwa mabao matatu tu katika mechi nne, wakati klabu hiyo ikiwa imeshinda mechi zake zote nne walizocheza za Ligi Kuu ya England wanashikilia usukani.

Lakini pia mshambuliaji mkongwe wa kiingereza Michael Owen amejumuishwa katika kikosi kilichokwenda Ureno huku wakiondolewa Mame Biram Diouf na Federico Macheda katika kikosi hicho.

Wakati Chelsea ndio timu itakayoelekea uwanja wa Old Trafford siku ya Jumapili, Sir Alex Ferguson atahitaji kutumia vizuri wachezaji alionao ingawa inaaminika atawatumia wachezaji wenye uzoefu zaidi dhidi ya timu iliyomaliza ikiwa nafasi ya pili katika Ligi ya Ureno msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment