Timu za Simba na Yanga zitaanza kuutumia Uwanja wa Azam Chamazi ulioko Mbande, Dar es Salaam wiki hii. Septemba 14 mwaka huu, Simba itakuwa mwenyeji wa Polisi Dodoma wakati siku inayofuata African Lyon itakuwa mwenyeji wa Yanga.
Viingilio kwa mechi zinazohusisha timu za Yanga na Simba kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 7,000 tu vitakuwa sh. 15,000 kwa jukwaa kuu na sh. 5,000 mzunguko.
Kwa timu nyingine za Dar es Salaam zinazotumia uwanja huo kiingilio kitaendelea kuwa kile kile cha sh. 10,000 jukwaa kuu na sh. 3,000 mzunguko.
Katika kutekeleza agizo la serikali la kutumia uwanja wa taifa kwa mechi mbili
Sasa mechi zitakazochezwa Uwanja wa Taifa ni
mechi namba 39- Azam vs Yanga (Septemba 18),
mechi namba 50- Simba vs Mtibwa Sugar (Septemba 25),
mechi namba 52- Yanga vs Coastal Union (Septemba 28)
mechi namba 58- Yanga vs Kagera Sugar (Oktoba 13).
Nyingine ni
mechi namba 62- Simba vs African Lyon (Oktoba 16),
mechi namba 65- Yanga vs Toto Africans (Oktoba 20),
mechi namba 72- Simba vs JKT Ruvu (Oktoba 22),
mechi namba 78- Yanga vs Simba (Oktoba 29)
mechi namba 86- Moro United vs Simba (Novemba 2).
Na mechi zifuatazo zitachezwa Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam, mechi namba 35- Simba vs Polisi Dodoma (Septemba 14), mechi namba 29- African Lyon v Yanga (Septemba 15), mechi namba 45- Yanga vs Villa Squad (Septemba 21), mechi namba 66- Simba vs Ruvu Shooting (Oktoba 19) na mechi namba 71- Yanga vs Oljoro JKT (Oktoba 23).
Uongozi wa Azam unaomiliki uwanja wa Chamazi tayari umekubali timu za Simba na Yanga kutumia uwanja huo kwa mechi hizo.
No comments:
Post a Comment