Monday, September 12, 2011

SIMBA WAIZIDI YANGA KIMAPATO


                             
Mchezo wa ligi kuu kati ya Azam na Simba uliochezwa Septemba 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam umeingiza shilingi milion sabini na mbili  laki moja nasitini na saba elfu, 72,167,000.

Watazamaji waliokata tiketi kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo walikuwa 21,129. Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 15,000, sh. 7,000, sh. 5,000 na sh. 3,000.

Viti vya bluu na kijani ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 viliingiza watazamaji 18,586, hivyo kuingiza sh. 55,758,000.

Wakati mchezo kati Yanga na Ruvu Shooting uliochezwa Septemba 10 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam umeingiza shilingi milion ishirinini na tatu, laki tatu na themaninini na nane elfu 23,388,000.

Watazamaji waliokata tiketi kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo walikuwa 6,566. Viingilio vilikuwa sh. 15,000, sh. 7,000, sh. 5,000 na sh. 3,000
........

No comments:

Post a Comment