Monday, September 12, 2011

YANGA YARUDI KWA VIONGOZI WA MATAWI


                                
Uongozi wa klabu ya yanga leo umekaa na viongo wa matawi yote ya jijini Dar es salaam na mikoa ya karibu ili kujadili na kulitafutia ufumbuzi suala la klabu hiyo kuendelea kushika mkia katika ligi kuu ya Tanzania bara.

Akizungumza na Anga la michezo msemaji wa klabu ya Yanga  Luis Sendeu amesema lengo la kuwaita vingozi hao wa matawi ni kuchangia mawazo kutokana na hali mbaya inayo wakabili wanajangwani hao.

Aliongeza kuwa timu hiyo tangu itwae taji la kagame timu hiyo haikufanya vizuri katika mchezo wowote ule zaidi ya kuibuka na sare.

Amesema umefika wakati wa timbe kufanya  kazi ya ziada ya kuongeza mazoezi kwa wachezaji wa klabu hiyo ya jangwani ili waweze kufanikisha hili.

Katika michezo yake baada ya kombe la kagame Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki na Polisi Dodoma ikafungwa 2-1, na ikacheza na EL Merekh ikafungwa 3-1 na mchezo wa mwisho wa maandalizi ni 3 -1.

Wakati jangwani wakitafuta njia ya kumaliza kilio cha kuharibu klabu ya simba inasema inashukuru kwa kupata sare katika mchezo wa jana dhidi ya Azam na kudai ni semhemu matokeo ya mchezo,

Akizungumza nami msemaji wa simba Ezekiel Kamwaga amesema sare hiyo imezidi kuweka simba kileleni mwa ligi hiyo ya Tanzania bara.

Lakini pia Kamwaga amesema wanaimani ya kufanya vizuri zaidi katika mchezo wao wa jumatano dhidi ya Polisi Dodoma na kuibuka na ushindi.

No comments:

Post a Comment