Maandalizi ya ligi TFF ngazi ya wilaya katika wilaya zote mkoani Iringa yanaendelea vizuri kwa kila wilaya huku wilaya ya mufindi ikionekana kutaka kuingia katika utata mara baaada ya mashindano ya wilaya hiyo ya Kambarage kuonekana yatavuruga ligi hiyo.
Akizungumza nami katibu mkuu wa IRFA mvela mahanji amesisitiza wilaya zote kumaliza ligi kabla ya November 15 ilikutoa nafasi kwa ligi ya mkoa kuanza mapema.
Baada ya katibu kuzungumzia hilo, msemaji wa chama cha mpira wa miguu wilayani Mufindi Kilipamwambu amekiri mashindano ya kombe la kambarage kuelekea kuvuruga mipango ya ligi hiyo.
Aliongeza kuwa hadi kufikia leo wanajitahidi kuhamasisha vilabu kuchukua fomu za ushiriki lakini vinasuasua.
Kwaupande mwingine Mvela amezika wilaya zote kukamilisha taratibu za uchaguzi katika wilaya zao na kukisifu cha cha soka Iringa mjini kwa kukamilisha michakato hiyo mapema.
No comments:
Post a Comment