Friday, September 9, 2011

MBEYA MJINI WA PATA MDHAMINI LIGI YA WILAYA


                                              
CHAMA cha soka wilaya ya Mbeya mjini (MUFA) kimesema kupatikana kwa ufadhili katika ligi ya taifa ngazi ya wilaya inayotarajia kuanza kutimua vumbi Septemba 17 mwaka huu kutaleta chachu ya ushindani tofauti na misimu iliyopita.

Uongozi wa MUFA umebainisha hayo  kufuatia kampuni ya usambazaji kompyuta ya Access Computer Ltd (ACL) ya jijini Mbeya kutangaza kudhamini ligi hiyo inayotarajia kushirikisha jumla ya timu 13.

Mwenyekiti wa Mufa, John Gondwe, amesema kampuni ya ACL itadhamini ligi hiyo kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi ambapo  mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi laki tatu na seti moja ya jezi na mpira mmoja.

Ameongeza kuwa kwa mshindi wa pili atazawadiwa shilingi laki moja na nusu na seti moja ya jezi na mpira mmoja ,ambapo  mshindi wa tatu atazawadiwa shilingi laki moja na seti moja ya jezi na mpira mmoja huku zawadi kwa mchezaji,mlinda mlango ,mwamuzi na kocha bora zikitarajiwa kutangazwa baadaye na kampuni hiyo.

Gondwe amesema lengo la udhamini huo kwa  chama na wadau kwa pamoja ni kuona ligi inapata msisimko tofauti na miaka ya nyuma ambapo timu zilizoibuka bingwa ziliishia kukabidhiwa kombe bila zawadi ya aina yoyote.

Kwa mujibu wa Gondwe timu ambazo zimethibitisha kushiriki ligi hiyo ni pamoja na Zaragoza FC,Black Scopion,Airpot Rangers, Eleven na Ilemi Shooting Stars Boys.

Timu zingine ni  Winers FC,Super Cargo,African Boys,Ilomba, Town Stars,Uyole Stars, Vijana FC na Iyunga Stars.

MARTESACKER AMPIGIA MAGOTI ADAMS


                                     
Mlinzi mpya wa klabu ya Arsena Per Matersacke hanaimani kama atakuwa bora zaidi ya beki wa zamani wa klabu hiyo  na timu ya taifa ya England, Tony Adams.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema Adams sio mtu anayetangazwa sana  na kuonyeshwa katika vituo mbalimbali vya televison lakini ni beki ambaye alikuwa mfano ndani ya Arsenal na dunia kwa ujumla.

Alizungumza hayo katika mtandao wa Arsenal amesema alikuwa akimshuhudia Adams akifanya vitu vikubwa kipindi yeye ana umri wa miaka 12 akiwa hana atadalili za kucheza kama Adams.

Adams mwenye umri wa miaka 45 sasa, ndio mchezaji pekee alieanza kucheza klabu hiyo toka katika kituo cha Arsenal mwaka 1980 na kupandishwa katika timu ya wakubwa mwaka 1983 na kumaliza maisha yake ya soka mwaka 2002 na kuweka rekodi Arsena kwa muda wa miaka 22 bila ya kuhama.
                        
Adams alicheza mechi 504 ndani ya Arsena na kufunga magoli  32 mashindano  yote aliyocheza.
Lakini pia Adams alitwaa mataji  manne ya ligi kuu. Mawili ya FA Cup na kombe la ligi mara mbili mataji yote hayo alichukua akiwa na bosi wa sasa Arsene Venga.

Kutokana na vigezo hivyo Martesakar anaimani ya kuwa ataongeza kipaji chake na atapata mafanikio ya juu zaidi katika soka akiwa na klabu hiyo.