Friday, August 26, 2011

FAGASON ALIA NA FA


                                   
Bosi wa manchester united Sir Alex Fagason ameibuka na kukishtaki chama cha mpira wa miguu nchini England kwa kutoitendea haki manchester united.

Bosi huyo aliewahi kufungiwa takriban mechi tano msimu uliopita kwa kosa  la kumkosoa mwamuzi waMartin Artinson na kutozwa kiasi cha paundi 30,000

Amekilalamikia chama hicho juu ya uteuzi wa wachezaji wake nane katika kikosi cha timu ya taifa ya England kitu ambacho anadai akizingatii maadili  ua ufundi katika soka na yanalenga kuikandamiza timu yake.

Bosi huyo mwenye umri wa miaka 69 amesem FA wanapaswa kugundua nani anafanya kazi kubwa katika utoaji wachezaji katika timu ya taifa na kuandaa utaratibu mzuri wa kwa vilabu hivyo lakini sio kuendesha kama hivi ilivyo.

Nyota ambao wamo ndani ya kikosi cha uingereza ni Wayne Rooney, Rio Ferdinand, Ashley Young, Michael Carrick, Tom Cleverley, Phil Jones, Danny Welbeck, Chris Smalling

Lakini pia mkurugenzi wa klabu hiyo David ameongeza kuwa FA haijali mchango wa United katika timu ya taifa na badala yake wanaipa adhabu kali za mara mara

No comments:

Post a Comment