Tuesday, August 23, 2011

NASRI AMALIZANA NA MANCHESTER CITY



Uongozi wa klabu ya Arsenal umetangaza kufikia makubaliano na Manchester city juu ya mauzo ya kiungo wake Samir nasri. 

Taarifa inasema kuwa kiungo amekosa safari ya kwenda nchini Italy kwatika mchezo wa pili wa klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Udinese na amelekea jijini Manchester kwaajili ya vipimo vya afya.

Nasri mwenye umri wa miaka 24, atajiunga na Arsenal kwa kiasi cha paundi milion 25 na kulipwa kiasi cha paundi 180000 kwa wiki.

Nyota huyo aliejiunga na Arsenal mwaka 2008 akitokea Olimpic Marsele amecheza michezo 126 na kufunga magoli 27 huku akiwa na magoli 15 katika msimu uliopita wa ligi.

Kwamaana hiyo Nasri anamfuata mfaransa mwenzake  Gaely Clich na Emanuel Adebayor ambao wote walijiunga na klabu hiyo wakitokea Arsenal.

No comments:

Post a Comment