Tuesday, August 23, 2011

NEWCASTLE UNITED NA ARSENA ZATOZWA FAINI



Shirikisho la mpira wa miguu nchini England FA limevitoza faini ya paundi 30000  vilabu vya Arsenal na Newcastle united kwa kosa la kushidwa kuwachunga kinidhamu wachezaji wao wakatika timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kwanza waligi kuu ya England.

Katika mchezo mchezaji wa Arsenal Gervas Koas Yao maarufu kama  Gervinho alikwaruzana na Joey Barton baada ya Barton kumchezea vibaya Gervinho.

Baada ya tukio hilo mwamuzi wa mchezo huo Piter Walton alimtoa kwa kadi nyekundu Gervinho kwa kosa la kujibu shambulizi na akampa kadi ya njano Joe Barton.

Mara baada ya kutolewa kwa maamuzi hayo vilabu vyotea vilikata rufaa na kutupiliwa mbali huku faini ikiwa imesimama kidete.

No comments:

Post a Comment