Thursday, August 25, 2011

ROBBEN AITAMANI BARCA


                  
Winga wa Bayern Munich  Arjen Roben  amesema kuwa anavutiwa na kuitumikia klabu bingwa barani Ulaya FC Barcelona .

Nyota huyo wa zamani wa Chelseana Real Madri ambaye kwasasa ana umri wa miaka 27 amesisitiza kuwa klabu hiyo haijatuma ofa yoyote kwake mbali na kuhusishwa na kutakiwa na klabu hiyo.

Katika maelezo yake Roben ameipaka shedo Barca kwa kusema ni klabu bora na anapaswa kuizungumzia haswa kwa kutaka kujiunga nayo kama inapatika nafasi.

Amesema kuwa yeye anafuraha zaidi katika maisha yake ndani ya Alianz Arena na hawezi kujitoa ghafla kwa sababu ya Barcelona.

No comments:

Post a Comment