Mshambuliaji wa Monaco Park Chu Young anajipanga kumalizana na Arsenal juu ya uhamisho wake ndani ya wikiend hii.
Nahodha huyo wa South Korea mwenye umri wa miaka 26 aliecheza michezo 91 ndani ya klabu hiyo ya ufaransa kwa sasa yupo njiani kufanya vipimo vya afya ndani ya maasaa 24 yajayo.
Kabla ya kufanyika kwa dili hilo tayari Monaco ilikubaliana na Lille juu ya uhamisho wa nyota huyo na tayari alishamaliza vipimo vya afya hayo yali elezwa na Rais wa Lille Michael Seydox .
Lakini kikwazo kimekuja baada ya bosi wa Arsenal Arsene Venga kupiga simu na kutangaza nia ya kumtaka nyota huyo aijungena washika bundu wa jiji la London.
Katika historia fupi ya mchezaji huyo wa Kikorea amezaliwa mwaka 1985 na amecheza michezo 91 ndani ya Monaco na kufunga magoli 25 ambapo katika klabu yake ya zamani ya FC Seoul Alicheza 69 na kufunga magoli 23.
Huku akiwa na rekodi nzuru ndani ya timu ya taifa kwa kucheza michezo 53 na kufunga magoli 17. Kumbuka pia Park alifunga goli la pekee katika kipigo cha magoli manne kwa moja dhidi ya Argentina kule afrika ya kusini katika fainali za kombe la dunia mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment