Monday, September 12, 2011

MEIRELES AILAA LIVERPOOL


                                
Kiungo wa kireno aliejiunga na klabu ya Chelsea mwishoni mwa kipindi cha usajili Raul Meireles ameshutumu klabu yake ya zamani ya Liverpool kwa kuvunja ahadi na kumlazimisha asaini mkataba mwingine.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema hakutaka kuondoka liverpool ila vitendo vya ndani ya klabu hiyo vimemfanya aamue kuondoka.

Amedai kwamba katika mkataba wake mpya liverpool ilimuomba asaini mkataba kwa kumuongezea malipo ya mshahara kwa asilimilia 100 ya malipo yake lakini Liverpool hakutekeleza hili.

Kiungo huyo wa kireno alijiunga na Chelsea kwa dau la paundi milion 12 mwishoni mwa mwezi uliopita ikiwa na mwaka mmoja tangu ajiunge na liverpool akitokea FC Porto.

Amesema hakutaka kuondoka liverpool kama wangetekela ahadi ila uaminifu ndio umemfanya kuchukua uamuzi wa kuhama.
Lakini pia Meireles amesema ahofii wa hana tatizo na kocha wa Chelsea Andre Vila Boas na kudai kuwa amekaa nae kwa muda mwezi mmoja katika klabu ya Porto na anaimani hajabadilika kwa kiasi kikubwa katika utendaji wake.

Akiwa liverpool amecheza michezo 35 na amefunga magoli  matano.
Wasifu wake.
  • Kwa mara ya kwanza amecheza timu ya taifa mwaka 2003 dhidi ya Boavista
  • Ameshinda mataji manne ya ligi na klabu ya porto kuanzia mwa 2005-2006 na kuendelea.
  • Amecheza michezo 47 ya timu ya taifa na kafunga goli katika mchezo dhidi ya korea kaskazini katika fainali zakombe la dunia mwaka 2010
  • Alichaguliwa na PFA kama mchezaji bora kwa uteuzi wa mashabiki wa nchini ureno mwaka 2010-2011

No comments:

Post a Comment