Monday, September 12, 2011

ROBERTO MANCINI ALIA NA UFUNGAJI


                                
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema kikosi chake hakina budi kucheza vizuri zaidi licha ya ushindi mwepesi walioupata dhidi ya Wigan kwenye uwanja wa Etihad.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa City kushinda magoli matatu kwa sifuri, mshambuliaji wa Manchester city, Sergio Aguero alifunga mabao yote matatu peke yake huku Carlos Tevez akikosa pelnati katika dakika ya 19 ya mchezo huo.

Mara baada ya ushindi huo ulioifanya City kufikisha pointi 12 ikiwa na michezo minne huku ikizidiwa na united kwa tofauti ya magoli matatu ambapo united inaongoza kwa kuwa na magoli 15.

Kocha wa Manchester city Roberto Mancini hakufurahishwa na matokeo hayo kutokana na wachezaji wake kukosa nafasi nyingi za magoli.

Amesema ni tatizo kubwa kwa timu kupata nafasi k15 na kuzitumia nafasi 3 ambapo kwa upande wake anaona mchezo unaweza kubadilika mwishoni na kubadili matokeo ya mchezo.

Amesema wakati mwengine ni vizuri kumaliza mchezo katika kipindi cha kwanza na hakuna budi kubadilika kwa sababu wameuanza mchezo vizuri sana msimu huu lakini msimu ni mrefu.

Aguero sasa ana jumla ya mabao sita ya kufunga msimu huu na licha ya Tevez kukosa penalti, Mancini alisema anaridhishwa na kiwango cha nahodha huyo wa zamani wa Man City.

Edin Dzeko alipumzishwa katika mechi hiyo dhidi ya Wigan wakati huu City ikijiandaa kwa mchezo wa Ligi ya mabingwa wa Ulaya siku ya Jumatano dhidi ya Napoli

No comments:

Post a Comment