Monday, September 12, 2011

ZA LEO TOKA MANCHESTER UNITED


                                   
Nahodha wa Bolton wonderes, Kevin Davies amemuomba msamaha Tom Cleverley baada ya kumfanyia rafu mbaya kumuumiza  mguu.

Mke wa Davies, Emma, aliandika kupitia mtandao wa twitter: Kwa wale wote waliochukizwa na taarifa hiyo. Kevin amezungumza na Tom Cleverley kwa simu kuwa ile ni bahati mbaya na Kamwe huwa hana nia ya kumuumiza mtu yeyote.
                                   

Rafu hiyo mbaya ilifanyika dakika ya tano ya mchezo wakati Manchester United walipoilaza Bolton mabao 5-0 katika uwanja wa Reebock stadium 

Kutokana na vipimo vya dakari wa nyota huyo imeripotiwa kwa nyota huyo atakuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja. Na atakosa mchezo kati ya England na Montenego na baadhi ya mechi za manchester united
                                 
Wakati huohuo Mshambuliaji wa manchester united Javier Alnandez Chicharito amesema kuongeza uwezo wake wa ufanisi uwanjani ni jambo la msingi  na anajitahidi arudi kuliko alivyokuwa  katika msimu wake wa kwanza katika ligi hiyo.

Alnandez alijiunga na klabu hiyo mwaka 2010 majira ya joto la usajili akitokea klabu ya Chivaz Guadalajara alianzakuonekana mwiba katika sufu ya ushambuliaji ambapo laifunga magoli magoli 13 katika michezo yakyote ya ligi kuu nchini uingereza.

Katika mchezo wa juzi wa ligi kuu Alnandez alianza mchezo wake wa kwanza akitoka katika majeraha na kufunga magoli mawili katika ushindi wa magoli matano kwa sifuri dhidi ya Bolton Wonderes.

Takribani wiki sita Alnandez alikuwa nje ya uwanja na nafasi yakuchukulia na kinda la United Dan Welbeck lakini aliendelea kusisitiza kufanya  vitu bora zaidi pindi atakapo kuwa uwanjani  ili kuonyesha umuhimu wake wa kusajiliwa na Farguson.

Akishukuru kupitia television ya Manchester united amesema anashukuru wa kushinda katika mchezo wake wa kwanza na magoli yake yanalenga kuleta ushindi na kudhihirisha kama wachezaji wanafanya kazi wakiwa uwanjani.

Wiki iliyopita mshambuliaji wa United Wyne Roony alisema atatoa ushirikiano wa kutosha kwa Chicharito kwa kucheza kama washambuliaji Pacha ili kurudisha heshima iliyopo kwa kuamini uwezo wa nyota huyo wa Mexico.

No comments:

Post a Comment