Tuesday, August 23, 2011

JAP HEYNKES ATAKI NYOTA WA ZIADA.


                                        
Bosi wa Bayern munich ya ujerumani Jap Henkes amesema hana mpango wa kumsajili mshambuliaji mwingine kwa kuziba pengo la Ivica Olic ambaye ni majeruhi kwa sasa.

Jioni ya jana mkurugenzi wa klabu hiyo ya nchini Ujerumani  Karl Heinz amesema Bayern ina mikakati madhubuti ya kufanya marekebisho ya pengo hilo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Olic ambaye ni raia wa Crotia atakuwa nje kwa muda wa wiki nane kutokana kusumbuliwa na majeraha ya nyonga.

Jap anamatumaini ya hali ya juu kwa kikosi alichonacho na kudai kuwa afikiri kama kukosekana kwa Olic kunaweza kuleta madhara makubwa katika kikosi chake.

ANZI YATHIBISHA UHAMISHO WA ETOO.




Klabu ya Anz Makachkala ya nchini Urusi imetangaza kufikia makubaliano na  Inter Milan juu ya Usajili wa mshambuliaji nguli wa Inter Samuel Etoo.

Etoo amevuma kwa muda mrefu kutakiwa na klabu hiyo ya kirusi nas asa tayari klabu hiyo imeweka hadharani kufanikiwa kwa makubaliano yao.

Katika taarifa ya klabu ya Anz Makachkala inasema kuwa nyota huyo atanunuliwa kwa dau la paundi milion 25 ambapo paundi milion 21 zitabaki milan.

Tayari Anzi inawakongwe kama Roberto Calos na Yur Zikov  toka Chelsea

NEWCASTLE UNITED NA ARSENA ZATOZWA FAINI



Shirikisho la mpira wa miguu nchini England FA limevitoza faini ya paundi 30000  vilabu vya Arsenal na Newcastle united kwa kosa la kushidwa kuwachunga kinidhamu wachezaji wao wakatika timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kwanza waligi kuu ya England.

Katika mchezo mchezaji wa Arsenal Gervas Koas Yao maarufu kama  Gervinho alikwaruzana na Joey Barton baada ya Barton kumchezea vibaya Gervinho.

Baada ya tukio hilo mwamuzi wa mchezo huo Piter Walton alimtoa kwa kadi nyekundu Gervinho kwa kosa la kujibu shambulizi na akampa kadi ya njano Joe Barton.

Mara baada ya kutolewa kwa maamuzi hayo vilabu vyotea vilikata rufaa na kutupiliwa mbali huku faini ikiwa imesimama kidete.

NASRI AMALIZANA NA MANCHESTER CITY



Uongozi wa klabu ya Arsenal umetangaza kufikia makubaliano na Manchester city juu ya mauzo ya kiungo wake Samir nasri. 

Taarifa inasema kuwa kiungo amekosa safari ya kwenda nchini Italy kwatika mchezo wa pili wa klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Udinese na amelekea jijini Manchester kwaajili ya vipimo vya afya.

Nasri mwenye umri wa miaka 24, atajiunga na Arsenal kwa kiasi cha paundi milion 25 na kulipwa kiasi cha paundi 180000 kwa wiki.

Nyota huyo aliejiunga na Arsenal mwaka 2008 akitokea Olimpic Marsele amecheza michezo 126 na kufunga magoli 27 huku akiwa na magoli 15 katika msimu uliopita wa ligi.

Kwamaana hiyo Nasri anamfuata mfaransa mwenzake  Gaely Clich na Emanuel Adebayor ambao wote walijiunga na klabu hiyo wakitokea Arsenal.

MORNHO KUTOZWA FAINI TENA



Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini Hispania RFEF limetangaza kumtoza faini kocha wa Real Madrid Jose Morinho kwa kosa la kukwaruzana na kocha msaidizi wa FC Barcelona Tito Vilanova wakati wa mchezo wapili wa fainali ya Supercup uliochezwa katika uwanja wa CAMP NOU.

Kamati hiyo imesema lazima yatoke maamuzi ya busara na uwajibikaji kwa kocha wa huyo wa kireno  na Vilano.

mchezo huo uliomalizika kwa  Barcelona kuifunga madrid kwa magoli 3-2 ulipeleke Morinho kumkwaruza machoni Vilanova na kusababisha vurugu kmwishoni mwa mchezo huo

baada ya kikao cha jana cha kamati hiyo, kilipitia picha zote zilizotumwa ambazo zinaonyesha uhalisia wa tukio hilo  

kamati imeamua kufuata kifungu cha 22.1 katika kumuwajibisha wa mwalimu huyo mwenye sifa ya ubwatukaji"